Inspiring  Women  Families  and  Communities

MAELEZO KWA WATUNZAJI

Watunzaji hutoa huduma ya bure ya utunzi na usaidizi kwa jamii au marafiki ambao wana hali za magonjwa sugu, akili punguwani, ulemavu, au walio wakongwe.

Ishar imetambua ya kwamba kutoa utunzaji, ufadhili na upendo ni wajibu muhimu zaidi wa Watunzaji na kwamba utunzaji kwa watu wa jamii yako ni kazi ngumu inayohitaji nguvu za mwili na hisia kadhalika. Tunatambua pia kwamba kuhamia nchi nyingine kunamaanisha kurekebisha na kuzingatia mtindo mpya wa maisha na mara nyingi kupoteza ufadhili wa jamii na familia. Katika nchi yako ungeliweza kupata usaidizi kutoka kwa marafiki na jamii katika kuwatunza jamaa wako. Hapa katika mji wa Perth, unaweza kutafuta ufadhili kutoka kwa mashirika mbalimbali na makundi ya utoaji huduma.

Ikiwa umekabiliana na matatizo ya kumudu maisha yako siku baada ya siku, kubaguliwa, kutengwa kijamii, ukosefu wa kazi, umaskini, ukosefu wa makaazi, maswala ya matatizo ya kiakili kama vile mfadhaiko, dukuduku, huzuni, hasira, kujistahi kwa chini au hata uchomvu wa mwili, usitaabike kwa kunyamaza.Usaidizi unapatikana.   Pamoja na kufikia huduma zifaazo na ambazo zipo kwa ajili ya kukusaidia katika jukumu lako la Uangalizi, ni muhimu kwako kuzingatia mtindo wa kudumisha afya bora, ambao utakupitisha katika siku hizi za majaribu na kuweza kupata matokeo mema ipasavyo.

Usaidizi Wa Watunzaji Wa Tamaduni Mbali-Mbali Na Imarishaji

Huduma ya uma inayozingatia juu ya mahitaji ya watunzaji wanaoshughulikia watu wenya matatizo ya jazba, kijamii, kidini, na kilugha kutoka tamaduni zote

HUDUMA ZA USHAURI
TIBAMAUNGO
MAELEZO YA AFYA KWA LUGHA MBALI-MBALI
HUDUMA ZA KLINIKI
WARSHA ZA KUTANGAZA USHAURI WA KIAFYA
VIKAO VYA UANGALIZI WA KIBINAFSI NA UDEKEZAJI
MADARASA YA KUFUNZA MAZOWEZI YA VIUNGO
MAKUNDI YA USAIDIZI WA TAMADUNI MBALI-MBALI
SHUGHULI ZA SANAA/UFUNDI NA BURUDANI
MAELEZO JUU YA HUDUMA ZA UKAAZI
UKALIMANI BURE WAPATIKANA :

MIRRABOOKA
MADDINGTON
MIDLAND
FREMANTLE

ILI KUZUNGMZA NA OFISA MSAIDIZI WA UTUNZAJI, TAFADHALI PIGA SIMU NAMBARI   9345 5335


Twitter FaceBook RSS RSS